Straika majeruhi wa Simba, Patrick
Kiongera, anatarajia kuondoka nchini ndani ya wiki moja kwenda India kwa ajili
ya matibabu.
Tayari daktari atakayemtibu ameishampangia siku
ya kuanza kazi hiyo, baada ya kupunguza kazi zilizokuwa zimembana.
Mmoja wa viongozi wa Kundi la Friends of Simba
(FOS), amesema uongozi wa Klabu ya Simba umeandaa dola 5,000 (Sh milioni 8.5)
kwa ajili ya matibabu hayo.
“Matibabu pekee ni dola elfu tano, uongozi wa
Simba umeandaa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya matibabu.
“Yamebaki mambo machache tu kabla ya Kiongera
kuondoka kwa ajili ya matibabu hayo na upasuaji wa goti kwa jumla,” kilieleza
chanzo.
Kiongera aliumia katika mechi ya kwanza ya Ligi
Kuu Bara baada ya kugongana na kipa Shabani Kado wa Coastal Union.
Simba imekuwa ikipwaya katika safu ya
ushambuliaji, hali ambayo imeufanya uongozi uanze kuhaha kupitia kamati ya
usajili kwa ajili ya kujiimarisha zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment