Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amesema
bao moja alilofunga mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi, lilikuwa ni ukombozi mkuu
kwake na Wanasimba.
Phiri raia wa Zambia amesema mfululizo was
are hadi kufikia sita ulikuwa ukiumiza miiyo ya wachezaji, makocha, viongozi na
Wanasimba kwa ujumla.
“Lilikuwa bao muhimu sana, ni moja tu lakini
lilikuwa na maana kubwa sana. Ni bao lililoikomboa mioyo yetu kutoka kwenye
maumivu makali,” alisema Phiri.
Baada ya sare sita mfululizo zilizosababisha
kuibuka kwa mzozo Simba, hatimaye timu hiyo ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu
Shooting.
Katika mechi hiyo, Okwi aliyekuwa msumbufu
kwa mabeki wa Ruvu, ndiye aliyefunga bao hilo pekee.
Phiri anatarajia kurejea kwao Zambia kwa
mapumziko baada ya Ligi Kuu Bara kusimama hadi mwishoni mwa Desemba.
Hata hivyo anatarajiwa kurejea mapema kwa
kuwa kutakuwa na mechi ya Bonanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment