Waamuzi
23 wa daraja la kwanza wakiwemo wenye beji la Shirikisho la Kimataifa la Mpira
wa Miguu (FIFA) wameteuliwa kushiriki semina itakayofanyika Novemba 16 mwaka
huu jijini Dar es Salaam.
Washiriki
wa semina hiyo ambayo pia itakuwa na mtihani wa utimamu wa mwili (physical
fitness test) wanatakiwa kuripoti Novemba 15 mwaka huu kwenye hosteli ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyopo Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume.
Wakufunzi
wa semina hiyo wanaotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni
Riziki Majala na Soud Abdi.
Waamuzi
watakaoshiriki semina hiyo ni Ahmed Juma Simba (Kagera), Arnold Bugado
(Singida), Charles Peter Simon (Dodoma), Dalila Jafari Mtwana (Zanzibar),
Ferdinand Chacha Baringenge (Mwanza), Florentina Zabron (Dodoma) na Frank John
Komba (Pwani).
Grace
Wamara (Kagera), Hellen Joseph Mduma (Dar es Salaam), Israel Mujuni Nkongo (Dar
es Salaam), Issa Bilali Ali (Zanzibar), Issa Haji Vuai (Zanzibar), John Longido
Kanyenye (Mbeya), Jonesia Rukyaa Kabakama (Kagera) na Josephat Deu Bulali
(Tanga).
Kudra
Omary (Tanga), Martin Eliphas Saanya (Morogoro), Mary Kapinga (Ruvuma), Mfaume
Ali Nassoro (Zanzibar), Mgaza Ali Kinduli (Zanzibar), Samwel Hudson Mpenzu
(Arusha), Soud Iddi Lila (Dar es Salaam) na Waziri Sheha Waziri (Zanzibar).
0 COMMENTS:
Post a Comment