Hatimaye aliyekuwa kipa
wa Orlando Pirates, Senzo Meyiwa amezikwa kwa heshima kubwa.
Meyiwa aliyekuwa pia
nahodha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ amezikwa kwao Durban.
Amezikwa kwenye makaburi
ya watu maarufu ya Chesterville karibu kabisa na alipozikwa aliyekuwa mwandishi
maarufu Nat Nakasa.
Mashabiki walijitokeza
kwa wingi kuuaga mwili wake katika Uwanja wa Moses Mabida mjini Durban.
Kipa huyo aliuwawa kwa
kupigwa risasi na watu wanaominiwa kuwa majambazi na tayari mtu mmoja
amekamatwa akituhumiwa kwa mauaji hayo.








0 COMMENTS:
Post a Comment