November 7, 2014


Mwanasheria maarufu nchini Damas Daniel Ndumbaro amefunguka na kutoa sababu tatu tu zilizochangia kuibuka uadui kati yake na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.

Katika mahojiano yake maalum na blogu ya SALEHJEMBE, Dk Ndumbaro amesema wakati akiwa kwenye Bodi ya Ligi alikuwa mmoja kati ya watu wanaosaini utoaji wa fedha.
“Kwanza kabisa baada ya kukamatwa kwa basi la TFF, Malinzi aliagiza fedha zitoke huku na kulipa basi hilo.
“Fedha alizotaka ni zile za Yanga za udhamini wa Azam TV kwa kuwa hawakuwa wamezichukua. Nikakataa kusaini, niliingia hofu kama Yanga wangezitaka fedha zao, tungezitoa wapi?
“Kwake Malinzi ikawa ni nongwa, akaelezwa azungumze na mimi, akakataa kwa madai yeye ni rais hawezi kumbembeleza mtu, zoezi likakwama.
“Mara ya pili, Malinzi tena akataka alituma wakaguzi wa mahesabu kupitia kampuni ya Whitehouse Coopers waje kukagua mahesabu ya bodi.
“Kanuni na katiba ya TFF inasema anayetakiwa kukagua mahesabu ya bodi ni ile inayokagua mahesabu ya TFF. Ile kampuni ambayo jamaa waliokuja walikuwa ni kabila la Wahaya, haikuwa inakagua mahesabu ya TFF.
“Nikaona Malinzi alikuwa anavunja katiba, sikutaka aingie sehemu isiyo sahihi. Nikaona nimsaidie asije akaingia pabaya, nikagoma pia.”
Dk Ndumbaro amesisitiza kuwa jambo la tatu ni taarifa za yeye kutaka kuwania urais wa TFF.
“Rafiki zake wa karibu, hasa wapambe waliomzunguka ndiyo wamekuwa na hofu kubwa kwamba nikigombea basi yeye ataanguka kwa kuwa wanatambua hawako makini.
“Sikuwahi kuwa na mpango huo, lakini kitu cha msingi hawapaswi kuhofia washindani. Ndiyo maana unaona wameamua kunifungia kienyeji.
“Nakuhakikishia, hakuna watu makini wanaoweza kufanya kama ilivyofanya TFF kwa kushirikiana na kamati ya nidhamu.
“Watu wote wameona, serikali imeshangazwa, wadau wamepinga hilo na hiyo ni sehemu nyingine ambayo inaweza kuwa kipimo sahihi cha kuonyesha wao si watu makini hata kidogo.”


6 COMMENTS:

  1. Kwahiyo moja ya vigezo vya kupewa tenda ya ukaguzi kwa makaampuni ya ukaguzi lazi mmiliki asiwe Muhaya? harafu kingine anasema malinzi alimlazimisha kusaini ili Pesa za Yanga zitoke, Je? yeye ni kiongozi wa Yanga? maana inavyo julikana Azam Tv inatoa Pesa kwa Vilabu kupitia Account zao, na ndio maana azam Tv waliwaambia Yanga kama akizitaka Pesa waandike barua Azam Tv hawawezi kuzitoa kinyemela, sasa hizo alizolazimishwa Ndumbalo ni zipi?

    jamni ndumbalo umeiharibu Simba na sasa unaenda TFF sababu tu ya Hao friends of Simba, tunajua yote haya ni kwasababu Dewj kanyimwa tenda ya kuuza vifaa vya Michezo vya timu ya Taifa,tu hakuna kingine, na endelea kutumika tu kaka haina shida, na nyinyi wandishi wa habari hizo rushwa mnazo endekeza zinaua mpira wa Tanzania kabisa, hebu kama kweli hampokei Rushwa habari zenu ni zakweli sio za kupewa? tuleteeni picha za maendeleo ya Uwanja wa Simba pale Bunju.

    ReplyDelete
  2. We salehe panga sijui! Ushauri wangu kwanza nenda kapige msasa wa elimu yako ili upate upeo zaidi! wewe si mwandishi uliye kwalifai bali ni mzugaji ebu jaribu kuwa makini na unachokuwa unaandika..wewe unaiona TFF tu huyo mtu anatafuta umaarufu... kila kukicha TFF... wewe salehe kaongeze upeo uko nyuma saana.. yaani habari za sport umeziwwka kidaku saaana... mwanzo ulianza vizuri naona sasa umepitiliza.... south africa kuna chuo kimoja kizuri saana mwambie mwajiri wako akupeleke ukasugue hiyo akili.. umefanya nisiwe napitia tena habari zako..azimeki sensi.. wee endelea kukopi tu kwenye magazeti ya spoti uingeleza ... the dail mail..ndiko unako kopi habari za spoti...please nimekusaidia mawazo yafuatilie! Una kiwango cha kuwa mwandishi...bali unakiwango cha kuandika tu. Una boa saana na habari za kila kukicha malinzi na ndumbaro ndio nani kwanza ndumbaro...

    ReplyDelete
  3. kaka saleh ally mimi sina shida na wewe kabisa, natofautiana na wenzangu kwamba wewe si mwandishi bora, hicho kitakuwa kichekesho, wala siwezi kukuita haujui lolote kwa kuwa eti umeandika habari za malinzi na ndumbaro maana sasa ndiyo ishu. mwenzangu aliyekujibu ambaye ana hasira kweli, naye maandishi yake yanaonyesha inabidi aongeze elimu ya mwandiko.
    swali langu kwako kwani hauwezi kujibu hizi comments, hata kama utaona wengine wanakuudhi lakini jibu ili tupate ufafanuzi kwa baadhi maana tuko tunaotaka kujifunza zaidi na hatuna maslahi na hatu jazba...tusaidie maana unapochangia halafu mtu kakaa kimya, kidogo inaudhi

    ReplyDelete
  4. JAMANI WENGINE TUNATAKA KUJUA UKWELI WA NDUMBARO NA MALINZI, KWENYE UANDISHI KUNA KITU KINAITWA FOLLOW UP, ASIYEJUA YEYE NDIYE ANGEENDA SHULE KUJIFUNZA. MNAKASIRIKA NINI, AU MNA MASILAHI NA TFF AU MALINZI.

    ReplyDelete
  5. kama unaona abari itakuumiza si uache kusoma au usifungue ha hahaha

    ReplyDelete
  6. Pengine ni kweli asemayo Ndumbaro,lakini kwa nini yasemwe wakati huu?
    Ungekuwa mwema kama ungefichua haya maovu kwa wakati.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic