November 7, 2014

RAIS WA SIMBA, EVANS AVEVA AKIWA NA MAKAMU WAKE, GEOFREY NYANGE 'KABURU'.

Uongozi wa Klabu ya Simba umelivaa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu kauli yao ya kuzitaka klabu kutojihusisha na wakili wa kujitegemea Damas Ndumbaro kupitia kampuni yake ya Maleta & Ndumbaro Advocate.


Rais wa Simba, Evans Aveva, amefunguka kuwa kwa upande wao bado wanaendelea kumsapoti Ndumbaro kwa asilimia 100 kwa sababu wao ndiyo waliomtuma na kudai kuwa watashirikiana naye kama kawaida katika masuala ya soka.

“Kamati iliyoshughulikia suala hilo ni huru na kwa upande wetu Simba tupo mstari wa mbele kuhusu suala hilo na tunamsapoti.

“Tutaendelea kumtumia Ndumbaro kama kawaida kwani tunatetea haki yetu na tunapinga vikali makato ya asilimia tano ya mapato.

“Hakuna waraka wowote tuliopewa klabu kuhusu jambo hilo,” alisema Aveva.

TFF ilitangaza kumfungia Ndumbaro kujihusisha na soka kwa miaka saba kutokana na kile kilichoelezwa kukiuka kanuni kadhaa za shirikisho hilo.


4 COMMENTS:

  1. Mtumieni tu si ndio aliwasaidia katika uchaguzi? na ndio kaboresha Simba mpaka sasa ina maendeleo? Uwanja upo, wachezaji wanalipwa vizuri, umoja Club pale ni shwari, kwani mnafikiri hatujui kuwa ninyi ndio mlimtuma akusanye sahihi za wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF ili zipigwe kura za kutokuwa na imani na Malinzi? kwani sisi hatujui kuwa Kasim Dewj kanyimwa tenda ya kuuza vifaa vya michezo vya timu ya taifa? endeeleni kuvuruga mpira wa tanzania ipo siku itajulikana tu Mungu yupo.

    ReplyDelete
  2. ajabu kweli, anayetaka kuiba fedha za mpira na anayetetea zisiibiwe yupi anayetaka kukuza mpira. sasa mnataka Malinzi aachiwe aibe ili mpira uendelee....kichekesho...

    ReplyDelete
  3. mimi pia nashangazwa sana na watu wanaoona Malinzi anaonewa, ukiangalia kisa anataka kuchukua fedha za klabu, ugomvi wake ni kukatazwa asichukue hizo fedha. halafu huyo mbwiga anamshilikisha mungu kwenye huu ujinga. Huyu bwana malinzi ndie anaua mpira maana tokea ameingia analumbana na kila mtu sasa...kila siku madudu na ujinga mpya, saleh wala usichoke wala usiogope na kama ukimuonea malinzi tutakueleza ukweli lakini kwa hili la sasa, mwambieni abadilike, wadau tumeishamchoka kabisa kabisa!!!!

    ReplyDelete
  4. JAMBO LA MSINGI HAPA NI KLABU KUMTETEA DOKTA NDUMBALO, PIA ALIWATETEA NA FEDHA ZAO MALINZI HAKUZIPATA. POINT TAKEN...
    MIMI NIMEFURAHISHWA NA KAULI YA AVEVA NA KAMA DOKTA NDUMBALO ANA MAKOSA, BASI KWINGINE. KWENYE KUZITETEA KLABU LILIKUWA JAMBO ZURI NA ALIKUWA NA HOJA KULIKO TFF...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic