Stand United imeendelea kuipa wakati mgumu Mbeya City baada ya kuichapa kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara.
Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, wenyeji walipata bao lao katika dakika ya 74. Kabla ya hapo, Stand United walipata penalti lakini wakashindwa kuitumia.
Kwa kipigo hicho, sasa Mbeya City imepoteza mechi nne msimu huu hali ambayo itasababisha hofu kwa mashabiki wake kuwa huenda haitakuwa na makali kama msimu uliopita.
Hata hivyo ligi bado mbichi, huenda ina nafasi ya kujirekebisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment