Danny Mrwanda ameendelea kusamba 'sumu' ya kuchana nyavu baada ya leo kuifungia bao pekee timu yake ya Polisi Moro wakati ilipoibuka na ushindi wa bao 1-0.
Polisi Moro imeifunga Prisons ya Mbeya katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, leo.
Licha ya Prisons kutawala kipindi cha kwanza lakini haikuweza kupata bao.
Kipindi cha pili kilikuwa cha Polisi Moro ambao mwisho waliibuka kwa kuizamisha Prisons kwa bao pekee la Mrwanda ambaye mechi iliyopita alikuwa shujaa kwa kufunga mabao mawili ya ushindi.
Mrwanda alianza kuchipukia akiwa na AFC ya Arusha, baadaye ikamchukua kabla ya kumuuza Polisi Rwanda na baadaye akaenda kukipiga Al Tadhamoun ya Kuwait hakafy akafunga safari hadi Vietnam.
0 COMMENTS:
Post a Comment