Beki kisigi Serge Wawa raia wa Ivory Coast
amefuzu vipimo vya afya tayari kuichezea Azam FC.
Wawa ambaye anakipiga El Merreikh ya Sudan
amefuzu baada ya kufanyiwa vipimo kwenye kliniki ya Ebtu Physical Therapy
United ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema
baada ya kufuzu vipimo hivyo, wanasubiri majibu kutoka kwa uongozi wa juu.
“Kuhusu vipimo, Wawa anaonekana yuko safi. Sasa
ni suala la uongozi wa juu kuamua. Bodi ya wakurugenzi tunaisubiri na mwisho
tutajua kama Wawa atasajili Azam FC au la,” alisema Iddi.
Azam FC imeamua kuimarisha safu yake ya
ulinzi huku ikiwa na mabeki visiki watatu ambao ni nahodha Aggrey Morris, Said
Morad na David Mwantika.
0 COMMENTS:
Post a Comment