Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic amewaliza
mashabiki wa soka nchini Sweden wakati akipokea tuzo yake ya tisa ya mchezaji
bora wan chi hiyo.
Zlatan alikuwa akimzungumzia kaka yake
aitwaye Sakpo ambaye alifariki dunia mwaka jana kwa ugonjwa unaoaminikakuwa ni
kansa.
Mazungumzo yake yaliwafanya watu wasimame na
kumpa heshima kwa kumpigia makofi.
Lakini wengine akiwemo mpenzi wake walishindwa
kujizuia na kumwaga machozi.
0 COMMENTS:
Post a Comment