Timu ya Azam FC iko katika
maandalizi kwa ajili ya kwenda nchini Zambia kucheza mechi za kirafiki.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar
Iddi amesema wako kwenye maandalizi.
“Tayari uongozi umeanza
kulifanyia kazi suala la safari. Likiwa tayari tutawataarfu na tumeanza
mawasiliano na timu za Zambia,” alisema.
Aidha, Jaffar alisema kesho
kutakuwa na mechi ya kirafiki kati ya Azam kikosi kikubwa dhidi ya Azam B.
Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment