Watani wa Jadi Simba na
Yanga watapata nafasi ya kubadili hadi wachezaji watano katika mechi ya
kirafiki ya Bonanza, maarufu kama Mtani Jembe.
Mkurugenzi wa Mashindano wa
TFF, Boniface Wambura amesema wamefikia uamuzi huo kuwa wachezaji wanaoruhusiwa
kuingia katika dakika 90 ni hadi watano kwa kila timu.
“Sub imeongezwa siku hiyo,
badala ya wachezaji watatu, itakuwa hadi wachezaji watano.
“Kama mechi itaisha ndani
ya dakika tisini bila ya kupata mshindi, basi zitapigwa penalti tano tano
kwanza.
“Kikubwa katika mechi hiyo
ni lazima siku hiyo mshindi apatikane,” alisema Wambura.
Mechi hiyo ya Bonanza
inasubiriwa kwa hamu kubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment