December 22, 2014


Baada ya kupokelewa kama mfalme, kiungo wa Stand United, Haruna Chanongo amegeuka kuwa kivutio kutokana na kujaza mamia ya watu kwenye Uwanja wa Kambarage ambao walifika kushuhudia vitu vyake katika mazoezi ya timu hiyo, juzi Jumamosi.


Kiungo huyo amepelekwa kwa mkopo Stand akitokea Simba lakini sasa ndiye anayeonekana kuwa mfalme wa Stand United, kila shabiki wa timu hiyo akiwa ameweka matumaini makubwa kwake.

Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo, Muhibu Kanu, alisema mashabiki wa Stand wameonekana kuvutiwa na Chanongo na juzi walifika uwanjani kwa wingi wakiwa na lengo la kumuona.

Kanu alisema kuwa, wamekuwa wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Kambarage na mashabiki wamekuwa wakijaa lakini tangu Chanongo aanze mazoezi Ijumaa na juzi Jumamosi, watu wamekuwa wakijaa zaidi.

“Tunamshukuru Mungu tunaendelea vyema na  maandalizi na wachezaji wote wapya wameshaanza mazoezi, akiwemo Haruna Chanongo, Khamis Thabiti na Abuu Ubwa lakini mashabiki wamekuwa wengi kupita kawaida, tofauti na siku za nyuma.

“Wengi wanataka kumuona Chanongo, hata hivyo tumeandaa mechi kwa ajili ya kuwatambulisha kwa mashabiki wetu kabla ya ligi kuanza tena, lengo ni kujifua zaidi na kuwa na kikosi imara na cha ushindani,” alisema.

  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic