PLUIJM |
Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans
van Der Pluijm, amewabadilisha namba kiungo wa timu hiyo, Nizar Khalfan na beki
wa kushoto, Edward Charles.
Pluijm alianza kuinoa Yanga juzi
Jumamosi baada ya kuingia mkataba wa mwaka mmoja na nusu akichukua nafasi ya
Mbrazili, Marcio Maximo aliyesitishiwa mkataba wake kutokana na kutokuwa na mwenendo
mzuri wa timu.
Katika mazoezi yaliyofanyika juzi
Jumamosi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola jijini Dar, Pluijm
alimchezesha Nizar kama beki wa kati huku Charles akichezeshwa beki wa kulia.
Yanga kwa sasa inajiandaa na mchezo wa
Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam unaotarajiwa kupigwa wikiendi ijayo kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar.
Alipotafutwa Pluijm
kutaka kujua kwa nini aliwabadilisha namba, akasema sababu ni
upungufu wa mabeki kutokana na nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuwa na
matatizo ya kifamilia huku Mbuyu Twite akisumbuliwa na majeraha.
“Cannavaro na Twite hawapo na
nilipowauliza Nizar na Charles kama wataweza kucheza nafasi zile wakasema wapo
tayari kufanya hivyo, ndiyo maana umewaona wapo katika nafasi hizo, napenda
kila mchezaji awe ana uwezo wa kucheza nafasi tofautitofauti ili kukifanya
kikosi kuwa kipana zaidi,” alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment