Kampuni ya ujenzi ya Fenway Sports Group itafanya kazi ya upanuzi
wa Uwanja wa Anfield, kitita cha pauni milioni 114 ndiyo kitakachotumika.
Liverpool imethibitisha utanuzi huo wa uwanja wake na unatarajia
kuanza Jumatatu.
Uwanja huo unatarajia kufikia watu hadi 53,500, na jukwaa kuu
litaongezwa hadi watazamaji 8,500.
Upanuzi huo unatarajia kukamilika kabisa wakati wa msimu wa 2016-17.
Inaelezwa baada ya uwanja kukamilika, utakuwa ukiipatia Liverpool
zaidi ya kitita cha pauni milioni 20 kila mwaka.
0 COMMENTS:
Post a Comment