Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza wachezaji
watakaotumika katika mechi ya Bonanza ya Nani Mtani Jembe kati ya Simba dhidi
ya Yanga lazima wawe wale waliosajiliwa kwa mujibu wa kanuni.
Yanga au Simba hazitaruhusiwa kumtumia mchezaji yoyote ambaye
hayuko kwenye usajili wakati wa mechi hiyo ya Oktoba 13 kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar.
Maana yake, Simba haitaweza kumtumia kiungo wake Mgambia, Omar
Mboob hadi hapo itakapomsajili.
Kama itamsajili, itawakosa mmoja kati ya Amissi Tambwe au Pierre
Kwizera ambao italazimika kuwatema.
Hadi sasa inaonekana Simba bado inamjaribu, hivyo haitakuwa lahisi
kupata uhakika wa kumsajili hadi Desemba.
Hata hivyo, Mboob atapata nafasi nyingine ya kuonyesha uwezo wake,
kesho kwenye Uwanja wa Taifa wakati Simba itakapoivaa Express ya Uganda.
0 COMMENTS:
Post a Comment