Kiungo mpya mkabaji wa Yanga,
Mbrazili, Emerson Roque, Jumamosi alikuwa jukwaani akishuhudia timu yake
ikipepetana na Waganda, Express FC, katika mchezo wa kirafiki, jambo ambalo mashabiki
wa Yanga walipinga kutomjumuisha kikosini.
Hata hivyo, Kocha wa Yanga, Marcio
Maximo, ameibuka na kutaja sababu ya kumuondoa kikosini katika mchezo huo kuwa
bado amechoka kwani alitumika sana katika ligi kuu ya nchini Brazili alikotokea
kwenye Klabu ya Bonscusessco inayoshiriki Ligi Daraja la Pili, lakini akaongeza
kuwa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Simba atakuwemo.
Maximo amewaondoa wasiwasi mashabiki ambao wanadhani nyota huyo pengine
anaumwa.
“Sikuweza kumtumia Emerson juzi, kwa
kuwa bado ana uchovu wa ligi, alihitaji kupumzika zaidi maana Ligi ya Brazil
imemalizika hivi karibuni na alikuwa akicheza mechi nyingi, kwa hiyo niliona ni
vema nikampa muda mrefu wa kupumzika kabla ya kuanza majukumu makubwa kwenye
mechi dhidi ya Simba,” alisema Maximo.
Roque ambaye anafananishwa na Yaya
Toure wa Manchester City, kutokana na uwezo wa kukaba na kufunga, mtihani wake wa kwanza ni kuwasimamisha
viungo machachari wa Simba, Emmanuel Okwi na Shaban Kisiga hapo Jumamosi.
0 COMMENTS:
Post a Comment