Mwandishi Wetu, Zanzibar
Habari nzuri kwa mashabiki wa Simba, kiungo mkabaji wa timu hiyo, Jonas Mkude, ameanza
mazoezi baada ya kupona malaria iliyomuweka nje ya uwanja kwa wiki moja kwa
ajili ya matibabu.
Kiungo
huyo alishindwa kumalizia mazoezi ya wiki iliyopita kwenye Uwanja wa TCC, Chang’ombe
jijini Dar es Salaam baada ya kutapika kabla ya kufanyiwa vipimo na kukutwa na
malaria na kuanza dozi.
Katika
mazoezi ya jana yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ualimu hapa Unguja,
Zanzibar kiungo huyo alionekana akianza mazoezi mepesi ya binafsi kukimbia
akiwa chini ya uangalizi wa daktari, Yassin Gembe.
Gembe alisema Mkude amepona kabisa na mechi ya kesho
Jumamosi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Yanga atakuwepo uwanjani kama kocha
ataamua kumtumia.
“Mkude
kama unavyomuona hii leo (jana) asubuhi ameanza mazoezi mepesi ya binafsi kwa
ajili ya kurudisha afya yake ya kawaida, ameanza mazoezi mepesi na baadaye
akafanya ya nguvu pamoja na wenzake.
“Ametokea
kwenye malaria, hivyo ni lazima aanzie na mazoezi mepesi ili hali ya kawaida
irejee, kocha akiamua kumtumia ni ruksa. Tofauti na Mkude hakuna majeruhi
mwingine,” alisema Gembe.
0 COMMENTS:
Post a Comment