Mshambuliaji Danie Mwarwada, maarufu Danny Mrwanda amekubali kwa asilimia mia kurejea Simba.
Mrwanda amekubali kurejea Simba baada ya kuzungumza na viongozi wa Msimbazi na ndani ya siku chache ataanza kuonekana katika kikosi hicho.
Mrwanda huyo ameonyesha uwezo mkubwa wa kupachika mabao, baada ya kuifungia Polisi Moro mabao manne katika mechi saba na alikuwa na mpango wa kurejea na kuichezea timu yake ya Dong Tan Long ya nchini Vietnam.
Mrwanda sasa ataungana na washambuliaji wengine Emmanuel Okwi,
Amissi Tambwe, Elius Maguli na Dan Sserunkuma anayetarajiwa kumalizana na Simba
wiki hii, katika kutengeneza safu ya ushambuliaji hatari zaidi kwenye Ligi Kuu
Bara.
Mrwanda amesema tayari ametua jijini Dar wakati tayari kumalizana na Simba kama watakuwa tayari.
Kuhusiana na mchezaji huyo, Kocha Patrick Phiri:
“Kwanza kabisa ninafurahi
kuona Mrwanda anarejea kwa mara nyingine kuja kuichezea Simba, ni mshambuliaji
mwenye uwezo mkubwa. Bado sijajua anasaini mkataba wa miaka mingapi na
ninafikiri itajulikana baada ya kutua nchini na kukutana na viongozi.
“Ninatarajia kuwa na safu nzuri ya ushambuliaji baada ya
kufanikiwa kumpata Mrwanda na Sserunkuma,” alisema Phiri.
0 COMMENTS:
Post a Comment