EMERSON AKISAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA KUICHEZEA YANGA MBELE YA MTAALAMU WA MAMBO YA IT NA MSEMAJI WA YANGA, BARAKA KIZUGUTO. |
Kiungo
Emerson De Oliveira Neves Roque leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia
klabu ya Young Africans baada ya benchi la ufundi kuridhika na uwezo wake,na
mchezaji mwenyewe kufikia makubaliano hayo ya kuwatumikia watoto wa Jangwani.
Baada
ya kufanya mazoezi kwa siku nne mfululizo chini ya makocha Marcio Maximo,
Leonardo Neiva na makocha wazawa Salavatory Edward, Shadrack Nsajigwa kwa
pamoja wameridhiswa na uwezo wake na kuomba apewe kandarasi la kuitumikia klabu
ya Young Africans.
Emerson
aliyekua akichezea katika timu ya Bonsucesso iliyopo daraja la pili kwenye
jimbo la Rio de Janeiro anachukua nafasi ya mshambuliaji Geilson Santos
"Jaja" ambaye ameshindwa kureje nchini kutokana na matatizo ya
kifamilia na kuomba klabu ya Young Africans imuache.
Kocha
wa Young Africans Marcio Maximo amesema wamerizishwa na uwezo na kiungo mkabaji
Emerson na kusema ataisaidia timu katika michuano mbali mbali ya Ligi na
Kimataifa.
Ujio
wa Emerson unafanya klabu ya Young Africans kufikisha jumla ya wachezaji watano
wa kimataifa, wengine wakiwa ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamis Kizza na
Andrey Coutinho.
0 COMMENTS:
Post a Comment