NDANDA FC |
Uongozi wa timu ya Ndanda FC umesema kuwa timu yao ipo imara na watahakikisha
wanaikalisha Mbeya City.
Kikosi
hicho leo Jumatano, kinatarajiwa kuanza safari ya kuelekea mkoani Mbeya, kwa ajili
ya maandalizi ya mchezo wao unaotarajiwa kuchezwa Ijumaa hii, ambapo wataondoka
na wachezaji 23.
Ofisa Habari wa Ndanda, Idrisa Bandari alisema kuwa,
wachezaji wote wako fiti kwa ajili ya mchezo huo.
“Kesho
(leo Jumatano), ndiyo tunatarajia kuanza safari ya kwenda Mbeya kwa ajili ya
maandalizi ya mchezo unaotarajiwa kuchezwa Desemba 26, dhidi ya Mbeya City.
“Wachezaji wetu wako fiti,
hakika tunaamini kuwa tutaibuka na ushindi mnono na wa kishindo,” alisema Bandari.
Ndanda inashika nafasi ya
13 kwenye ligi hiyo ikiwa na pointi sita, ambapo itavaana na Mbeya City ambayo
inashika mkia ikiwa na pointi tano.
0 COMMENTS:
Post a Comment