December 22, 2014



Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amesema anaithamini sana ndoa yake aliyofunga hivi karibuni na ana mapenzi makubwa na mkewe.


Lakini suala la kazi kuhusiana na Simba ni muhimu na analipa kipaumbele ndiyo maana ameamua kukatisha fungate.

Akizungumza kutoka Kampala, Uganda, Okwi alisema amefanya hivyo kutokana na heshima kubwa pia anayoipa klabu yake ya Simba.

"Kweli nimeamua kukatisha fungate, nitarudi Dar es Salaam kuiwahi mechi ya ligi kuu dhidi ya Kagera.

"Baada ya hapo nitaomba ruhusa ili nirudi kuendelea na ratiba ya fungate," alisema.

"Natamani kushirikiana na wenzangu kwa kuwa najua tunahitaji pointi tatu za Kagera, ni timu ngumu na umoja wetu unahitajika," alisema.

Okwi amefunga ndoa ya kimila, halafu ndoa ya dini ya Kikristo itafungwa Julai, mwakani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic