Azam FC imesema kocha wao, Joseph Omog, amefurahia tu kupangwa na El Merreikh katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kocha huyo ambaye awali alishawahi kukutana na
timu hiyo kipindi cha nyuma akiwa amedai anaifahamu timu hiyo hivyo hana hofu.
Azam ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza
michuano hiyo imejipanga kuhakikisha inafanya vyema baada ya kusajili wachezaji
imara na inatarajiwa kuanza karata yake dhidi ya Wasudan hao kati ya Februari
13-15 mwakani, ikiwa kwenye ardhi ya nyumbani.
Ofisa habari
wa timu hiyo, Jaffar Iddi alisema kocha wa timu hiyo anaendelea na mazoezi kama
kawaida na hata baada ya ratiba kutoka alionyesha hali ya kawaida na kuwaondoa
hofu wachezaji na viongozi.
“Kocha amefurahia sana ratiba hii na kudai ni
nzuri kwetu kwani anaifahamu vyema Al Merreikh na aliwahi kukutana nayo kwenye
michuano ya Kagame mwaka huu, akiwa anatufundisha, hivyo haimpi shida.
“Sasa hivi anaendelea kukipanga kikosi chake
ili kuhakikisha kinafanya vizuri kwenye mchezo huo ili tufanikiwe kuvuka raundi
ya kwanza,” alisema Jaffar.
0 COMMENTS:
Post a Comment