December 31, 2014


Simba imetua Zanzibar salama, tayari inajiandaa kwa ajili ya mechi yake ya kesho dhidi ya Mtibwa Sugar katika michuano ya Mapinduzi.



Hata hivyo, hadi leo asubuhi, Simba walikuwa hawajui kama wancheza kesho dhidi ya Mtibwa.

Kocha Msaidizi, Selemani Matola ambaye amekabidhiwa kikosi aliwanoa wachezaji wake kwa mazoezi magumu.

"Kweli hatukujua tuna mechi kesho, ratiba tuliyokuwa nayo inaonyesha tunacheza Ijumaa tarehe mbili. Ndipo tulipoambiwa kuna mabadiliko.

"Lakini waandaaji hawakuwa wametupigia kututaarifu. Baada ya kusikia hivyo nikaanza kuwatafuta na kugundua ni kweli," alisema Matola kwa masikitiko.

Waandaaji wa michuano ya Mapinduzi hawakuwahi kuwataarifu Simba kwamba wamefanya mabadiliko ya ratiba tofauti na taarifa ya awali waliyokuwa wamezipa timu.


Simba iko Kundi C, lenye timu za Mtibwa Sugar, Mafunzo na JKU.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic