December 31, 2014


Simba itaanza michuano ya Mapinduzi bila ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza zaidi ya wanne.



Kwanza ni kipa Ivo Mapunda aliyekwenda Mbeya kwenye arobaini ya kifo cha baba yake.

Wengine ni Waganda wanne, ambao ni Emmanuel Okwi aliyepewa ruhusa kwenda kumalizia fungate. Simon Sserunkuma, Juuko Murishid na Joseph Owino.

Mchezaji pekee wa kigeni ambaye yuko na Simba kwa sasa ni Simon Sserunkuma.

Tayari Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola amesema mchezaji ambaye hakuwepo kwenye mazoezi ya leo pale TCC Club Chang'ombe, hana nafasi ya kucheza mechi ya kesho ya ufunguzi wa Mapinduzi Cup dhidi ya Mtibwa Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic