December 9, 2014


Yanga imekamilisha kila kitu katika suala la makubaliano na mshambuliaji Kpah Sherman raia wa Liberia.

Sasa kilichobaki ni vipimo vya afya na akifuzu, atasajiliwa kwa mwaka mmoja.

Yanga imechukua uamuzi huo baada ya kuachana na mshambuliaji Mkongo wa AS Vita ambaye ameeleza ana mpango wa kwenda Ulaya.

Lakini pia imeelezwa mshambuliaji huyo ana mpango wa kujiunga na TP Mazembe.
Sherman amekuwa aking’ara nchini Vietnam na sasa Cyprus Kaskazini.

Amekuwa akifanya vema katika timu ya Cetinkaya TSK.
Akiwa na timu hiyo, aliwahi kufunga mabao matatu katika mechi tatu.
Hadi katikati ya msimu alikuwa na mabao nane na anatarajia kuwasili leo nchini.
Iwapo atatua leo, atafanyiwa vipimo vya afra ili kupata uhakika, akifuzu anaanza kazi mara moja.


Hata hivyo imeelezwa ana mkataba wa miezi minne na klabu yake na Yanga inalazimika kuuvunja kwa kulipa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic