December 9, 2014


Mashabiki wa Simba wameonyesha kushitushwa sana na habari za kusajiliwa kwa mshambuliaji Danny Mrwanda ambazo ziliandikwa jana kwa mara ya kwanza kwenye blog hii.

Baadhi ya wasomaji kupitia namba 0658 939769 inayomilikiwa na blog hii, walituma ujumbe wakihoji kama ni kweli au maigizo.

Baadhi walitumia email ya salehkubwa@gmail.com wakihoji kama tukio hilo ni sahihi.

Mrwanda amejiunga na Yanga kwa mwaka mmoja, siku chache baada ya kuwa na taarifa kwamba Simba imekaribia kumsajili.

Lakini baadaye Simba ikatangaza kusimamisha kumsajili baada ya kugundua hakuwaeleza ukweli.
Jambo hilo liliwafanya Yanga wachangamke kwa kuwa Kocha Marcio Maximo alisisitiza anamhitaji.

Uongozi wa Simba uliamua kuachana na Mrwanda kwa madai hakuwa mkweli kwa kuwa mwanzo aliwaeleza yuko huru lakini siku chache Polisi Morogoro wakawapigia simu wakidai chao.

Kwa kuwa Simba hawakuwa tayari wamemsajili, walihoji na wakaambiwa lazima Polisi walipwe. Jambo ambalo liliwafanya waone Mrwanda hakuwa mkweli, wakasitisha na kumtaka amalizane na Polisi ili arejee kumalizana na Simba.

Hapo ndipo Yanga wakaingia kati na kuchangamkia dili kabla ya kumnasa mshambuliaji huyo mwenye mabao manne.


Kutokana na hali hiyo, mashabiki hao wameonyesha kukerwa kwa kuwa wanaamini kikosi chao kinahitaji washambuliaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic