December 9, 2014


MAYWEATHER AKIWA NA RAPA HUYO PAMOJA NA MKEWE.

Bondia Floyd Mayweather ameshindwa kumshawishi rapa Earl Hayes asimuue mkewe.


Rapa huyo alimpigia simu Mayweather kutumia mfumo wa FaceTime unaowawezesha wanaowasiliana kuonana na kumueleza anataka kumuua mkewe Stephanie Moseley.
HAYES
Mayweather alianza kazi ya kumshawishi asifanye hivyo, lakini huku Mayweather akishuhudia kupitia simu, rapa huyo alimmaliza mkewe.
Baada ya hapo alizungumza na Mayweather kabla ya yeye pia kujimaliza.

Jirani wa eneo high-end  jijini Los Angeles waliwapigia simu polisi.

Polisi walifika eneo la tukio na kulazimika kuvunja mlango na kukuta wote wakiwa wamefariki dunia kwani baada ya kummaliza mkewe, rapa huyo naye alijitwanga risasi.
Mkewe alikuwa mmoja wa wacheza shoo na waimbaji kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali.

CHRIS BROWN ALIFANYA SHOO NA MAREHEMU, ALIPOSIKIA KIFO CHAKE AKAANDIKA HIVI KWENYE MTANDAO, KWAMBA ANASIKITIKA, WALIFANYA KAZI SIKU CHACHE KUMBE NDIYO ULIKUWA MWISHO WA BINTI HUYO. MWISHO AKATOA POLE KWA FAMILIA ZOTE ZA MAREHEMU.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic