Mshambuliaji
wa Man City, Sergio Aguero amesema anataka kufanya vema zaidi katika mechi
dhidi ya Arsenal, Jumapili.
Raia
huyo wa Argentina alikaa nje ya uwanja zaidi ya wiki tatu kutokana na kuwa
majeruhi.
Aguero
alirejea uwanjani katika mechi dhidi ya Everton ambayo iliisha kwa sare ya bao
1-1.
Lakini
amesema anaamini ushindani mkubwa katika mechi dhidi ya Arsenal itakuwa ni
changamoto ya kujituma zaidi ndiyo maana amekuwa akifanya mazoezi kwa juhudi
zaidi.
“Ninaamini
itakuwa ngumu, lakini napenda ushindani ili nifanye vizuri zaidi,” alisema.








0 COMMENTS:
Post a Comment