Yanga itashuka dimbani leo Jumamosi kumenyana na Ruvu Shooting katika mchezo wa
Ligi Kuu Bara lakini staa wa Yanga, Simon Msuva, ameandaliwa beki maalum wa
kuhakikisha hafurukuti, huyo siyo mwingine bali ni George Michael.
George
alikuwa tishio msimu uliopita ambapo alikuwa akiwadhibiti vizuri washambuliaji
wengi wakiwemo Amissi Tambwe na Didier Kavumbagu huku akitumia nguvu nyingi
kupambana.
Beki
huyo aliwahi kunukuliwa akisema kuwa amekuwa akipiga ‘pushapu’ 100 kwa siku,
hali ambayo alisema ilimsaidia kuwazima mafowadi.
Msemaji
wa Ruvu, Masau Bwire, ameliambia gazeti hili kuwa, beki huyo amerejea na tayari
ameshacheza baadhi ya mechi, huku akijinadi kuwa ndiyo atakuwa na kazi ya
kuzima wasumbufu wa Yanga, akimtaja Simon Msuva kwa kuwa ndiye ambaye yupo
kwenye kiwango kizuri.
“Msuva
atawasumbua wengine ila siyo sisi, George amerudi na atakuwepo, huyu ndiye dawa
ya wasumbufu siku zote na ndiyo kazi yake uwanjani,” alisema Bwire.







0 COMMENTS:
Post a Comment