Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho, amefunguka kuwa hajawa na mawasiliano
na kocha wake wa zamani aliyekuwa anakikinoa kikosi hicho, Marcio Maximo ambaye
ni Mbrazili mwenzake.
Uongozi
wa Yanga ulimfungashia virago Maximo mwishoni mwa mwaka jana kwa madai kuwa
alishindwa kuijenga timu vizuri huku pia akipoteza mchezo wa Nani Mtani Jembe
kwa mabao 2-0 dhidi ya Simba ambapo nafasi yake imechukuliwa na Mholanzi, Hans
van Der Pluijm.
Ikumbukwe
kuwa, Maximo ndiye aliyemleta nchini Coutinho pindi alipotangazwa kuwa kocha wa
timu hiyo huku akimleta pia msaidizi wake Leonardo Neiva ambapo wote
walitimuliwa siku moja pamoja na Wabrazili wengine, Emerson Roque na Geilson
Santana ‘Jaja’.
Coutinho amesema
hajawasiliana na Maximo tangu kocha huyo alipoondoka nchini Desemba, mwaka jana
ambapo kwa sasa ni takribani mwezi umefika.
“Sijawasiliana
naye tangu alipoondoka hapa Tanzania na hii yote inatokana na yeye kubadilisha
namba yake ya simu lakini nikiipata nitamtafuta kwani yeye ni kama ndugu yangu,”
alisema Coutinho.







0 COMMENTS:
Post a Comment