Unajisikiaje, kuona mpira
wa Tanzania leo uko hivi tena katika karne hii?
Picha zinaonyesha mchezaji
wa Polisi Dodoma akikimkimbiza mwamuzi wa mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza dhidi
ya Toto African.
Mwamuzi huo alilazimika
kukimbia kwenye majukwaa ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambako
aliokolewa na mashabiki waliompa kipigo mchezaji huyo.
Alimkibiza mwamuzi huyo
baada ya kumpiga uwanjani lakini alipokimbia, aliona haitoshi akaendelea
kumkimbiza.
Hii ndiyo soka ya Tanzania,
bado wachezaji wanakimbiza waamuzi na kuwapiga.
Kweli kama wanakosea,
sehemu sahihi za kuwapa adhabu zipo. Vipi wakimbizwe kama wizi? Hii ni aibu
kubwa ka mpira wa Tanzania ambao ndiyo bado unavaa ‘nepi’ kutokana na udogo
wake.









0 COMMENTS:
Post a Comment