January 15, 2015


Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ametamba kwamba wataichapa Yanga katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara, Jumamosi.


Masau litakuwa ni jambo la ajabu kama wao watashindwa kuifunga Yanga ambayo inapewa sifa nyingi na vyombo vya habari.

"Timu yenye imefungwa na JKU na kutolewa kwenye michuano ya Mapinduzi. Sasa unafikiri timu kubwa kama Ruvu Shooting itashindwa kuifunga.

"Hivyo watu waje waone namna ambavyo tutaiathiri Yanga ambayo nasisitiza, ni timu ya kawaida tu," alisema.

Mechi hiyo itakuwa ni ya pili kwa Kocha Hans van der Pluijm katika Ligi Kuu Bara tokea arejee Jangwani.

Mechi yake ya kwanza baada ya kurejea Tanzania, Pluijm aliingoza Yanga kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Azam FC.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic