January 15, 2015



Kipa mkongwe Ivo Mapunda ambaye aliingizwa katika dakika ya 90 kuikoa Simba kwenye mikwaju ya penalti wakati wa fainali za Kombe la Mapinduzi anasema alijua lazima atapangua au kudaka angalau penalti moja.


Mapunda alisema wakati ameambiwa angie kuchukua nafasi ya Peter Manyika, alijua ana jukumu zito na aliapa angelitekeleza.

"Penalti si kazi lahisi, ujuzi wa kipa lakini ujuzi wa mpigaji. Nilitaka angalau nipangue mbili ikishindikana hata moja," alisema.

Kipa huyo ambaye alipata umaarufu mkubwa katika Ligi Kuu Kenya wakati akiichezea Gor Mahia kutokana na upanguaji wa mikwaju ya penalti, aliisaidia Simba kubeba ubingwa wa Mapinduzi baada ya kupangua penalti ya Vicent Barnabas.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic