Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema wala haoni faida ya wachezaji wa kulipwa katika kikosi cha Yanga.
Kifaru ameisifia Mtibwa Sugar na kusema ni timu bora yenye wazalendo wengi.
"Hiki ndiyo kikosi haswaa cha Watanzania. Utaona tulipo, soka letu na tunakimbilia kwenda fainali ya Mapinduzi.
"Utaona uchezaji wetu si wa kubahatisha. Hauwezi kutulinganisha na timu nyingine kama Yanga ambayo ina wachezaji wengi wa kigeni ambao hawana msaada.
"Sisi tunaamini tunakwenda fainali, kama anakuja Simba au Polisi Zanzibar, itatukuta hivyo," alisema Kifaru akionyesha kujiamini.
"Mimi naamini tunakutana na timu changa ambayo haiwezi kutuzuia kusonga hadi fainali. Sisi tutakata tiketi ya fainali."
Yanga iling'olewa na JKU katika hatua ya robo fainali baada ya kuchapwa bao 1-0 lililowaacha hawaamini kilichotokea.
0 COMMENTS:
Post a Comment