January 9, 2015



Mshambuliaji Emmanuel Okwi anatarajia kutua leo nchini na kuungana na wenzake visiwani Zanzibar.


Okwi alipewa ruhusa na uongozi wa Simba kwenda kumalizia fungate ambalo alilikatisha siku chache baada ya kuoa.

Msemaji wa Simba, Humfrey Nyansio amethibitisha kuwa Okwi anatarajia kuingia nchini leo.

"Ni kweli anakuja leo Dar es Salaam na baada ya hapo ataungana na wenzake Zanzibar," alisema Nyansio.

Taarifa nyingine zilieleza Okwi atatua na ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda kabla ya kupanda ndege ndogo kwenda Zanzibar kuungana na wenzake ambao kesho watacheza mechi ya Kombe la Mapinduzi hatua ya nusu fainali.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic