Baada ya kiungo mshambuliaji wa Real Madrid,
Cristiano Ronaldo, kuibuka Mchezaji Bora wa Dunia wa 2014, Kocha Mkuu wa timu
ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mholanzi, Mart Nooij, ameibuka na kusema
kuwa yeye kura zake alipiga kwa wachezaji watatu akiwemo nyota huyo.
Alitaja listi yake ya aliowapigia kura kuwa ni
Arjen Robben (Bayern Munich), ya pili kwa Lionel Messi (Barcelona) na tatu kwa
Cristiano Ronaldo, ambaye alikuwa akiitetea.
Kwa upande wa makocha, Nooij alichemka kwani
katika listi yake alikuwepo Carlo Ancelotti (Real Madrid) ya pili ilikwenda kwa
Louis van Gaal (Manchester United) na ya mwisho Pep Guardiola (Bayern Munich)
wakati Fifa wamempa kocha wa Ujerumani, Joachim Low.
Nooij alisema aliwapigia wachezaji hao
kutokana na kutambua umahiri na uwezo wao ambao ni wazi wanafanya vyema na siyo
wababishaji wanapokuwa uwanjani, japo uwezo hauwezi kufanana moja kwa moja.
“Kura yangu ya kwanza nilimpigia Arjen Robben
na wa pili alikuwa ni Lionel Messi na wa mwisho alikuwa Cristiano Ronaldo.
“Upande wa makocha nilimpa Carlo Ancelotti
(Real Madrid), ya pili ilikwenda kwa Louis van Gaal (Manchester United) na
nilimalizia kwa Pep Guardiola (Bayern Munich),” alisema Nooij.







0 COMMENTS:
Post a Comment