Uwezo unaoendelea kuonyeshwa na kiungo
chipukizi wa Simba, Ibrahim Ajibu, umemkuna kiungo wa timu hiyo, Shaban Kisiga
na akatamka wazi kuwa mchezaji huyo si wa kuendelea kuwepo kwenye ligi ya
Tanzania kwa muda mrefu.
Ajibu ambaye amesajiliwa na Simba mwanzoni mwa
msimu huu akitokea Polisi Moro, amekuwa gumzo kwa sasa, hasa baada ya
kufanikiwa kuonyesha kiwango cha kuvutia kwenye Kombe la Mapinduzi huko
Zanzibar.
Kisiga alisema kuwa Ajibu si mchezaji mwenye
uwezo wa kawaida bali ni mchezaji anayefahamu soka kiuhalisia, hivyo mchezaji
kama huyo anapaswa kufikiria kucheza soka la kulipwa mapema mno na si kuendelea
kuwepo kwenye ligi ya Bongo.
“Ni mchezaji mzuri, anavutia sana akiwa
anacheza mpira, mchezaji kama huyo hastahili kuendelea kuwepo hapa Tanzania kwa
muda mrefu, hawa ni watu wa kucheza nje ya nchi soka la kulipwa, anatakiwa
kuangalia zaidi nje kuanzia sasa na si kuendelea kuzunguka katika timu za
Tanzania.
“Lakini pia kama akijitunza na kujithamini,
akizipuuzia anasa na mambo mengine yasiyo na msingi, akifuata misingi ya soka,
naamini atafika mbali zaidi,” alisema Kisiga.








0 COMMENTS:
Post a Comment