Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amewashangaa wanaosema kuwa
mshambuliaji wake, Mrundi, Amissi Tambwe hawezi kuwa mfungaji bora katika Ligi
Kuu Bara, msimu huu.
Tambwe
ambaye amejiunga na Yanga akitokea Simba ikiwa ni siku moja kabla ya dirisha
dogo la usajili kufungwa Desemba 15, mwaka jana, alikuwa mfungaji bora wa Ligi
Kuu Bara msimu uliopita kwa kufunga mabao 19 akiwa na kikosi cha Simba.
Pluijm amesema anavyomuona Tambwe ni
mshambuliaji anayejiamini na mwenye nguvu ambaye analijua vizuri goli kwa hiyo
msimu huu ana asilimia kubwa za kubeba tuzo ya ufungaji bora.
“Tambwe
ni mshambuliaji ambaye anajiamini, ana nguvu, pia analijua goli lilipo na msimu
uliopita alifanikiwa kutwaa tuzo ya upachikaji mabao, sasa kwa nini msimu huu
ashindwe kufanya hivyo?” alihoji Pluijm.







0 COMMENTS:
Post a Comment