Kocha Pep Guardiola wa Bayern Munich amewatabiria wapinzani wake wakubwa Borussia Dortmund watarejea kwenye chati.
Guardiola amesema wakali hao wana nafasi ya kurejea na kushangaza wengi.
"Hivi karibuni kutakuwa na mabadiliko na Dortmund watarejea kwenye nafasi za juu katika msimamo wa ligi.
"Hilo linawezekana kabisa, kupanda na kushuka inawezekana katika soka," alisema akiwa mjini Doha, Qatar ambako Bayern imeweka kambi kujiandaa na mzunguko wa pili wa Bundesliga.
Mwendo wa Dortmund umekuwa wa kusua kupindukia katika Bundesliga.








0 COMMENTS:
Post a Comment