Barcelona imefanikiwa
kuibuka na ushindi katika mechi yao ya kwanza ya robo fainali ya Copa del Rey.
Shujaa wao ni Lionel Messi
ambaye alifunga bao katika dakika ya 85.
Mechi hiyo ilikuwa ngumu
kutokana na wageni Atletico Madrid kuonyesha wamepania kusonga mbele.
Atletico inayoongozwa na
Fernando Torres imefikia hatua ya robo fainali baada ya kuing’oa Real Madrid.
Mechi ya pili mjini Madrid
ndiyo itakayoamua nani amesonga mbele kati ya Barcelona au Atletico.
0 COMMENTS:
Post a Comment