| MGOSI AKIMTOKA KIPA PETER MANYIKA WA SIMBA NA KUIFUNGIA MTIBWA SUGAR... |
Hassan Mgosi, ambaye amekuwa na rekodi nzuri ya kuzifunga Simba na
Yanga, amemtaja beki kisiki wa Yanga, Kelvin Yondani ‘Cotton’ kama mtu aliyempa
mbinu za kuwatoka mabeki wanaokamia, enzi wakiwa pamoja Simba.
Mgosi amesema kuwa mbinu alizopewa na Yondani na Juma Nyosso ambaye
sasa yupo Mbeya City, enzi walipokuwa Simba, zimemsaidia katika kuwapita mabeki
wa timu kubwa, hasa za Simba na Yanga.
“Wakati tukiwa Simba, Yondani na Nyosso walikuwa wakifanya kila
liwezekanalo kuhakikisha sifungi mazoezini, walikuwa wakicheza kwa kunikamia
haswa na si utani, hali ile niliichukulia ‘serious’ nikawa nafanya juu chini
ili nifunge, kumbe ilikuwa ikinijengea ujasili wa kutomuogopa beki yeyote hasa
wanaokamia mastraika.
“Kwangu ulikuwa kama wosia maana nimekuwa nikifunga katika mechi za
kukamia tofauti na nyingine,” alisema Mgosi ambaye yupo Unguja na timu yake kwa
ajili ya Kombe la Mapinduzi.







0 COMMENTS:
Post a Comment