SIKU moja baada ya uongozi wa Simba kutangaza kuachana na kipa Juma
Kaseja, sasa unalazimika kupambana na kesi mpya dhidi ya kiungo mshambuliaji
Emmanuel Okwi.
Kupitia mwanasheria wake, Kampuni ya Agaba Muhairwe & Co
Advocates ya Kampala, Uganda. Okwi amefungua kesi akitaka Yanga imlipe kitita
cha jumla ya dola 62,000 (zaidi ya Sh milioni 107).
Mgawanyo wa madai hayo umegawanywa mara mbili, ukianza na dola 50,000
ambazo Okwi anaidai Yanga aliposajili ikiwa alilipwa nusu yake.
Pili, mshahara wake, dola 12,000 ambao pia hakulipwa na Yanga. Jumla
inakuwa dola 52,000.
Tayari Agaba Muhairwe & Co Advocates wamewasilisha barua yenye
kumbukumbu namba AM/129/ea kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia
Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Haki za Wachezaji.
Barua hiyo ya Januari 7, kopi mbili, moja imewasilishwa kwa Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji na nyingine kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Mwanasheria huyo wa Okwi amesisitiza kwamba hawatafungua kesi yoyote
kwa kuwa wanatoa hadi Februari 15 kuwa wameishalipwa fedha hizo.
Sehemu ya barua hiyo inaonyesha barua ya juzi inakumbushia barua
nyingine kama hiyo ambayo kampuni hiyo ya mwanasheria iliitoa na kutaka Okwi
awe amelipwa hadi Desemba 15, mwaka jana lakini haikufanyika.
Maana yake, iwapo Yanga watashindwa kufanya hivyo watakuwa tayari
kufungua kesi ya madai kuhakikisha wanapata fedha zao na haina ubishi
watakwenda Fifa ambayo wameisha itaarifu kuhusiana na deni hilo.
Okwi aliondoka Yanga baada ya uongozi kumtema katika hatua za mwisho
za usajili wa dirisha dogo na Simba ikamsajili, hali iliyozua tafrani kubwa.
Baadaye TFF ilimpitisha Okwi kuichezea Simba na Yanga haikuwa imekubaliana na
uamuzi huo.
Kopunovic: Waleteni hao Yanga
Na Sweetbert Lukonge, Zanzibar
BAADA ya kikosi cha Simba kufanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe
la Mapinduzi kwa kishindo, kocha mkuu wa timu hiyo raia wa Serbia, Goran
Kopunovic, ametamka wazi: “Waleteni hao Yanga.”
Jumatano iliyopita, kocha huyo aliyejiunga na Simba hivi karibuni akichukua
mikoba ya Mzambia, Patrick Phiri, alikuwa ni mwenye furaha kubwa baada ya
kuishuhudia timu yake ikipata ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Taifa Jang’ombe.
Matokeo hayo yamempa jeuri ya kutamka hivyo kwa kusema kuwa yupo
tayari kupambana na timu yoyote ikiwemo Yanga ambayo imeonekana kufanya vizuri
pia.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kopunovic alisema kuishuhudia timu
yake ilipocheza na Mtibwa Sugar yeye akiwa jukwaani, aligundua mambo mengi ya
kiufundi yaliyokuwa na upungufu.
“Vijana wanajitahidi sana kuzingatia maagizo yangu, jambo ambalo
linanipa matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mashindano haya.
“Kuna mabadiliko makubwa tofauti na nilivyowakuta, hivi sasa wanaweza
kupambana na timu yoyote ile kwenye mashindano haya na kuibuka na ushindi, hata
hiyo Yanga wataifunga kama tukikutana nayo,” alisema Kopunovic.







0 COMMENTS:
Post a Comment