Kitendo cha
kiungo Shabani Kisiga kimesababisha kifo cha shabiki mmoja wa Simba jijini Dar
es Salaam.
Kisiga alikosa
penalti wakati wa fainali ya Kombe la Mapinduzi jana dhidi ya Mtibwa Sugar
ambayo iliisha kwa Simba kushinda kwa mikwaju 4-3.
Kukosa kwa
Kisiga kulifanya Simba iwe katika hatihati ya Simba kulikosa kombe hilo na
inaelezwa mtu huyo alianguka na kuzimia na baadaye alipoteza maisha.
Awali ilielezwa
ni eneo la Mburahati, wengine wakaeleza ni Tegeta.
Mtu mmoja
alihojiwa na redio ya E FM na kusema aliyefariki dunia ni baba yake mdogo.
“Hakuwa na
tatizo lolote la afya, hata wakati anakwenda kuangalia mpira kwenye runinga
alikuwa safi.
“Baadaye
tukaletewa taarifa kwamba alianguka baada ya Kisiga kukosa penalti,” alisema.
Taarifa
zinaeleza mwili wa marehemu utasafirishwa kesho kwenda kwao Mbeya.







0 COMMENTS:
Post a Comment