Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeizuia timu ya Polisi Mara kutumia Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma kwa mechi zake za Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
kuanzia leo mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
Uamuzi huo
umechukuliwa kutokana na matukio ya vurugu na uvunjifu wa amani ambayo yamekuwa
yakitokea kwenye mechi za FDL zinazochezwa kwenye uwanja huo, ikiwemo ile ya
Jumamosi iliyopita dhidi ya Mwadui ya Shinyanga ambapo waamuzi walipigwa.
Kamati
zinazohusika zitakutakana hivi karibuni kupitia matukio yote ya utovu wa
nidhamu kwenye FDL, na hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika ikiwemo na viwanja
ambavyo vimekuwa na sifa ya vurugu.
Vyama vya mpira
wa miguu vya mikoa vina wajibu wa kutoa ulinzi wa kutosha viwanjani wakati wa mechi.







0 COMMENTS:
Post a Comment