Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm
amesema anataka nafasi wanazotengeneza katika kikosi chake zitumite kutengeneza
mabao.
Pluijm raia wa Uholanzi amesema
itakuwa ni kazi bure kama watatengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia.
“Soka ina kawaida ya kuendelea
kukumbusha na wakati mwingine kufundisha jambo lilelile kwa mara nyingine tena.
“Lakini ninachotaka ni nafasi za
kufunga mabao zitumike. Tunapotengeneza nafasi bila kuzitumia ni kazi bure,”
alisema.
“Tayari nimezungumza na wachezaji
wangu mara kadhaa na nitaendelea kuwakumbusha ili kuhakikisha kunakuwa na
mabadiliko katika hilo,” alisema.
Yanga imekuwa na kikosi
kinachopoteza nafasi nyingi za kufunga licha ya kushinda baadhi ya mechi kwa
idadi nzuri ya mabao.
“Hata zile tulizoshinda kwa mabao
manne, tulistahili kushinda zaidi,” alisisitiza Pluijm.







0 COMMENTS:
Post a Comment