Fernando Torres amefunga mabao mawili na
kuiwezesha Atletico Madrid kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Real Madrid katika
mechi ya Copa del Rey.
Kwa sare hiyo ndani ya Santiago Bernabeu,
maana yake Madrid imeng’olewa kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya kuwa imepoteza
kwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ikiwa ugenini.
Licha ya kuwa na wachezaji nyota zaidi
duniani, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale, Madrid ilishindwa kuonyesha cheche
na kumzuia Torres kufanya mambo yake.
Torres amerejea Atletico akitokea AC Milan
iliyomnunua kutoka Chelsea kabla ya kuamua kumpeleka Atletico kwa mkopo.















0 COMMENTS:
Post a Comment