| SANANI AKIZUNGUMZA... |
Waandishi mbalimbali wa
vyombo vya habari, wakiongozwa na wa gazeti la michezo la Championi na Azam
TV,walionyesha mapenzi ya dhati walipoamua kumtembelea Masoud Sanani.
| LUKONGE (KULIA) AKIWA NA MUWA NA MBULA WA AZAM TV |
Sanani ni kati ya waandishi magwiji nchini hasa katika michezo na sasa ni
mgonjwa baada ya kupooza upande mmoja wa mwili wake.
Waandishi hao walimtembelea
nyumbani kwake eneo la Bububu mjini Zanzibar.
Waandishi hao walikuwa
kwenye michuano ya Mapinduzi, kwa pamoja walifika kumuona gwiji huyo ambaye
amewahi kufanya kazi katika makampuni ya Business Times akiwa na gazeti la
Spoti Starehe na Dar Leo kabla ya
kuhamia Mwananchi ambako pia alifanya kazi katika Mwanaspoti.
| LUKONGE WA CHAMPIONI AKISALIMIANA SANANI... |







0 COMMENTS:
Post a Comment