Mashabiki wa Feyenoord ya Uholanzi wamezichapa
vilivyo na askari polisi wa mji wa Roma nchini Italia.
Mashabiki hao walikuwa mjini humo kuiunga mkono
timu yao ikikipiga dhidi ya Roma katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Polisi wmefanikiwa kukamata mashabiki 33 katika
vurugu hizo jana.
Mashabiki hao wa Feyenoord wanaokadiriwa kufikia
6,000 walikabiriana vilivyo na askari hao katika eneo la vivutio vya utalii wa
jiji la Roma.
Mashabiki kadhaa walijeruhiwa pamoja na askari polisi kutokana na vurugi hizo zilizodumu kwa zaidi ya saa nane.

























0 COMMENTS:
Post a Comment