February 3, 2015


 Rais wa Simba, Evans Aveva ametua katika mazoezi ya Simba akiongozana na 'swahiba' wake, Kassim Mohammed Dewji maarufu kama Gwiji katika mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja ulio kwenye kambi ya Jeshi eneo la Dege nje ya jijini la Dar.



Pamoja na kuangalia mazoezi, Dewji na Aveva waliwaita chemba Kocha Mkuu, Goran Kopunovic na msaidizi wake, Selemani Matola na walionyesha kukubaliana na kazi yao huku mkono wa Dewji akionyesha alama ya dole, kama vile anakubaliana na kazi yao.

Aveva na Dewji walifuatilia kwa umakini mkubwa kila kilichokuwa kikiendelea kabla ya kutoa maoni yao kwa benchi hilo la ufundi ambalo lina kazi kubwa Jumamosi dhidi ya Coastal Union.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic